Nilipoteza fahamu kwa siku nne-Akuku Danger azungumza

Muhtasari
  • Mchekeshaji huyo alifichua kuwa aliambiwa mapafu yake yanashida na pia alikuwa ameshikwa na homa ya mapafu katika mchakato huo
Magonjwa yaliyokuwa yameshambulia Akuku Danger yafichuliwa
Magonjwa yaliyokuwa yameshambulia Akuku Danger yafichuliwa
Image: INSTAGRAM// SANDRA DACHA

Mcheshi Akuku Danger amezungumza kuhusu ugonjwa uliomfanya alazwe hospitalini kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Akuku Danger alizaliwa na Sickle Cell Anemia, alipata matatizo ya kifua mnamo Desemba, na kusababisha kulazwa katika Hospitali ya Nairobi West.

"Ninaujua mwili wangu na kwa kuwa nimekuwa na anemia ya sickle cell tangu kuzaliwa, najua kunapotokea tatizo. Nilipojipeleka hospitalini nilikuwa na matatizo ya kupumua

Nililazwa mara moja na baadaye nilihamishiwa Nairobi West Hospital ICU ambapo nilipoteza fahamu kwa siku nne,"," Akuku aliambia Standard.

Mchekeshaji huyo alifichua kuwa aliambiwa mapafu yake yanashida na pia alikuwa ameshikwa na homa ya mapafu katika mchakato huo.

Alilazwa kwa takriban miezi miwili katika Hospitali ya Nairobi West na alitoa shukrani kwa marafiki, familia na watu wema waliosaidia kulipia bili kubwa ya matibabu.

“Kupitia paybill tulifanikiwa kukusanya karibu Sh3milioni ambazo zililipa bili yangu ya kwanza ya matibabu. Msaada ulikuwa mwingi

Kwa sasa nina salio la Sh1.3milioni ambalo ninapaswa kufuta katika siku 60 zijazo," alisema, na kutoa wito kwa umma kusaidia kwa njia yoyote iwezekanavyo.

Mnamo Februari 8, Akuku Danger aliondolewa kwenye kituo hicho baada ya kulipa bili ya karibu Sh 3 Milioni.