Maisha ya mapenzi ya Betty Kyallo ni yale ambayo Wakenya wanajali sana.
Mjasirimali huyo ambaye hivi majuzi aliachana na wakili, Nick Ndeda akiwa kwenye mahojiano na Plug TV, alifunguka kuhusu iwapo yuko kwenye mahusiano mengine.
Alipoulizwa kama anachumbiana alisema,
"Kwa sasa mimi ni mzuri sana. Mwaka huu ninatimiza miaka 33 kama Yesu na ninataka kuhakikisha kuwa ninaenda kutimiza ndoto zangu zote. Nia yangu ni biashara na kutafuta pesa. kwa binti yangu."
Aliendelea na kusema;
"Huwezi kuamuru ni nani utakayempenda. Kwa sasa siko katika nafasi hiyo kwani ninaangazia biashara, binti yangu na familia yangu. .Huwezi kuchagua unayempenda.Unampenda mtu anayeendana na nafsi yako.Niko sawa niko single na ninajifurahisha.Nataka umakini nilioweka kwenye mapenzi uende kwenye biashara yangu."
Alikariri kuwa alikuwa mahali pazuri maishani mwake, akibainisha kuwa;
"Nafikiri nimefurahi sana kukutana na watu na kupamba moto na ndoto zangu. Unajua wakati mwingine unapokuwa kwenye uhusiano unajisahau lakini nahisi hivi sasa nipo mahali ambapo ninazingatia kile ninachofanya." unataka. Si mbaya. Niko sawa!"