Nilikuwa navalia nguo za mama yangu-Kinuthia afichua haya

Kelvin Kinuthia
Image: Mercy Mumo

Mtayarishaji maudhui na nyota wa Tiktok Kelvin Kinuthia anasema mapenzi yake ya kujipodoa yalianza alipokuwa mvulana mdogo.

Akiwa kwenye mahojiano na  RadioJambo, nyota huyo maarufu alisema alipenda sana kuonekana kama mwanamke.

"Mimi ni mtoto wa mama yangu katika familia ya watoto watatu. Mimi ni kitinda mimba katika familia yetu, wengine ni dada

Siku zote niliwapenda wanawake waliojipodoa, nilitaka kujipodoa vizuri. Ningevaa nguo za mama yangu nikiwa na umri mdogo," Alizungumza Kinuthia.

Alipoulizwa kama mamake alikuwa na tatizo na hilo, Kinuthia alisema hakuwa na tatizo.

Anafurahia jambo hilo hata sasa. Nilimpoteza baba yangu nilipokuwa mdogo. Mama yangu aliingilia pengo na wakati pekee nilihisi kuathirika ilikuwa shuleni nilipo nitaulizwa kuhusu baba yangu."

Amesema kuwa hataki kufichua jinsia yake kwa sasa.