logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Maneno hayawezi kuelezea upendo wangu kwako!" Diamond amsherehekea bintiye Tiffah Dangote

Siku ya Wanawake Duniani Diamond aliwasherehekea Mama Dangote, Tiffah Dangote, Esma Platnumz na Zuchu.

image
na Samuel Maina

Burudani09 March 2022 - 09:43

Muhtasari


  • •Jumanne wakati dunia yote iliadhimisha siku ya wanawake duniani staa huyo wa Bongo aliwasherehekea mamake Sanura Kassim, dadake Esma Platnumz, bintiye Tiffah Dangote na msanii wake Zuchu.

Nyota wa Bongo Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha uhusiano mzuri kati yake na watoto wake na Zari Hassan.

Licha ya kuwa na jumla ya watoto wanne wanaojulikana, mara nyingi Diamond ameonekana kuwapendelea zaidi watoto wawili ambao alipata na mwanasoshaiti huyo kutoka Uganda.

Jumanne wakati dunia yote iliadhimisha siku ya wanawake duniani staa huyo wa Bongo alitumia fursa hiyo kusherehekea mamake Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote, dadake Esma Platnumz, bintiye Tiffah Dangote na msanii wake Zuchu.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond alipakia picha za wanne hao na kuziambatanisha na emoji za upendo.

Baba huyo wa watoto wanne aliambatisha picha ya bintiye na ujumbe, "Maneno hayawezi kueleza upendo wangu kwako Tiffah Dangote."

Diamond hakusherehekea baby mama wake yeyote ama mpenzi wake wa zamani yeyote katika siku hiyo maalum kwa wanawake.

Licha yake kumsherehekea Zuchu, mapema mwaka huu Diamond alipuuzilia mahusiano ya kimapenzi naye huku akidai kuwa yuko kwenye mahusiano na mwanadada mwingine asiye maarufu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved