Nameless aorodhesha mambo atakayo mfanyia Wahu anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ujumbe wake alimshukuru mkewe kwa kuwa naye maishani, na kumfanya kuwa mtu bora.

Huku msanii Wahu Kagwi akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, mumewe Nameless kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameorodhesha mambo ambayo atamfanyia siku hii maalum.

Kupitia kwenye ujumbe wake alimshukuru mkewe kwa kuwa naye maishani, na kumfanya kuwa mtu bora.

Wawili hao wameonyesha mfano mwema kwa wanandoa, huku wakiwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10.

Moja wapo ya mambo ambayo msanii huyo aliorodhesha ni kwamba atakuwa dereva wa mkewe kwa siku, atampikia na chochote kile atataka.

Huu hapa ujumbe wake;

"Birthday Gal♥️♥️♥️MamaTumiso🧐... Obviously Today anything unasema kwa nyumba is the law... Tunajua🙄🤪...ni utamaduni wa Mathenge, take advantage...ni leo tu.😊. Fam nisaidieni kumtakia rafiki yangu heri njema siku yake ya kuazaliwa. wewe ni baraka katika maisha yangu.. Character development umenipatia weuh 😅😅😅...mimi ni mtu bora kwa ajili yako😁... HAPPY BIRTHDAY babe...

I am at your service, I will be your Uber driver, cook ,masseuse, boy toy, mubaba chochote unataka😅😅 .. uliza utapewa, lakini ni ya Leo tu🧐. #ReadyToServe," Nameless Aliandika.