"Umejizolea mali ambayo wanaume wa miaka 69 wanatamani" Akothee amsifia Betty Kyalo

Muhtasari

•Akothee amesema kwamba mtangazaji huyo tayari ameweza kujipatia utajiri mkubwa akiwa na umri wa ujana tu.

•Akothee alisema kwamba mtangazaji na mfanyibiashara huyo hajabarikiwa kwa urembo tu ila kwa hekima pia.

Mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee amempongeza mtangazaji mashuhuri Betty Kyallo kwa mafanikio makubwa ambayo ameweza kujizolea.

Akothee amesema kwamba mtangazaji huyo tayari ameweza kujipatia utajiri mkubwa akiwa na umri wa ujana tu.

"Msichana mdogo mwenye ndoto kubwa na mafanikio makubwa. Katika umri wa miaka 30 tayari umejizolea mali ya kutosha ambayo wanaume wengi katika miaka 69 hutamani tu," Akothee alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto watano alimtakia Betty Kyallo kheri za siku ya kuzaliwa anapotimiza miaka 33. 

Akothee alisema kwamba mtangazaji na mfanyibiashara huyo hajabarikiwa kwa urembo tu ila kwa hekima pia.

"Wewe ni malkia kweli! Kheri za siku ya kuzaliwa Betty Kyallo mwituasa," Akothee aliandika.

Betty alipendezwa na ujumbe wa Akothee na kumshukuru huku akimtaja kama dadake mkubwa na mwanamke mzuri.

Mtangazaji huyo alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Machi 15.