logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Producer Master Jay asema Tz imeipiku Kenya kwenye burudani

Producer Master Jay akiri kwamba Tanzania ipo mbele ya Kenya katika muziki.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 March 2022 - 07:19

Muhtasari


  • • Producer huyo alisema kwamba wasanii wa Tz wanajituma sana jambo ambalo limewafanya kuibuka kidedea.
  • • Alikiri kwamba kipindi cha nyuma kidogo, Kenya ilikuwa mbali sana ila mambo yamebadilika sasa.
Instagram, KWA HISANI

Producer mkali wa muziki kutoka Tanzania Joachim Marunda Kimaryo almaarufu Master Jay amesema kwamba Tanzania imeipiku pakubwa Kenya katika gemu la burudani.

Akizungumza katika mahojiano na wanahabari, Master alisema kwamba uchachari na kujituma kwa wasanii wa Bongo kumepelekea wao kuwa kifua mbele.

Alikiri kwamba kipindi cha nyuma, Kenya ilikuwa imeishinda Tz katika uzalishaji wa muziki ila kwa sasa mambo yamebadilika.

"...Acha nikuambie kitu na hata Kenya wenyewe wanajua. Kitambo sisi Tanzania tulikuwa tunatoa video kama za harusi, yaani Kenya ilikuwa mbali sana ila kwa sasa mambo yamebadilika sanaaa," Master Jay alisema.

Kulingana naye, Tanzania ipo mbele ya mataifa ya Uganda na Kenya katika upande wa muziki.

Aidha, alikiri kwamba kwa sasa wasanii wa Tanzania wanapigana kuhakikisha kwamba wanakubalika katika soko la ughaibuni jambo ambalo anaamini litatimia hivi karibuni.

Master Jay ambaye aliwahi kuwa msanii pia, alisema kwamba sasa ni nafasi ya chipukizi zaidi kutamba katika sekta hiyo na kuwa hatojihusisha kwenye masuala ya uimbaji kwa sasa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved