logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mapenzi kikohozi! Zari anengua maungo kwa kibao kipya cha Diamond

Alionekana akisakata densi huku wimbo huo wa kimapenzi wa Diamond ukiendelea kucheza.

image
na Samuel Maina

Burudani29 March 2022 - 12:02

Muhtasari


  • •Zari alisikika akiucheza wimbo namba mbili kwenye albamu ya FOA, 'Somebody' ndani ya gari lake.

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri kutoka Uganda, Zari Hassan ameonekana kuvutiwa na EP mpya ya aliyekuwa mumewe, Diamond Platnumz. 

Katika kanda ya video ambayo alipakia Instagram, Zari alisikika akiucheza wimbo namba mbili kwenye albamu ya FOA, 'Somebody' ndani ya gari lake. 

Mama huyo wa watoto watano alionekana akisakata densi huku wimbo huo wa kimapenzi wa Diamond ukiendelea kucheza.

Zari ambaye ana watoto wawili na Diamond alionekana kufahamu vizuri maneno ya wimbo huo kwani pia yeye alikuwa akiuimba ulipokuwa unaendelea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved