Mashabiki wamemshambulia Harmonize baada ya kupakia video ya jumba lake kwenye mtandao wa Instagram.
Harmonize alipost video iliyokuwa ikionyesha ukubwa na ukali wa jumba hilo lenye madhari mazuri.
Chini kwa chini kilikuwa kinacheza kibao chake cha #Bakhresa ambacho mle ndani kama anajisifia kwamba yeye ni msanii mkubwa ambaye haitaji kutumia kifua ili watu kumkubali.
Aidha, alisikika mwishoni mwa video hiyo akisema kwamba "waambie tunamiliki hili jengo."
Kauli hiyo inakisiwa kulenga wapinzani wake ambao wamekuwa wakimpiga vita hasahasa Diamond Platnumz ambaye kulingana na Harmonize alikuwa anataka kusambaratisha muziki wake.
Vilevile baadhi ya mashabiki nao walitupa cheche kali wakisema kwamba 'Jeshi' alikuwa akifanya hayo kutokana na presha ya EP ya Diamod Platnumz, huku akitafuta kila namna kusalia kileleni.
"😂😂😂 kiki zote lakini FOA inazidi kupepea. Kesho DIAMOND anaachia video ya pili, hadi akifika video ya 10...KUNDU BOY atakuwa ameshatuonyesha hadi makalio yake," shabiki alisema.
Baadhi pia walisema kuwa wasanii hao wakubwa wanaonyesha majumba yao kama njia moja ya kuwakatisha tamaa na kuwafanya wao kuonekana kwamba hawatii bidii maishani.
"Yaaani hawa vijana wanakeraaa.wanatufanya si tuonekane hatujui kutafuta hela. Yaaani mi na degree zangu hii nyumba naishia kuiona kwenye video daaaaah😢😢😢😢," shabiki mmoja aliandika.