Baby mamas wawili wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Tanasha Donna wamethibitisha wazi kwamba hakuna uhasama wowote kati yao.
Licha ya kuwa wote waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond, Hamisa na Tanasha wameonyeshana upendo mkubwa kupitia mtandao wa Instagram.
Siku ya Jumapili, Tanasha alipakia picha yake na mwanawe anayefanana na Diamond kama shilingi kwa ya pili, Naseeb Juniour.
Mobetto ambaye pia ana mtoto mmoja na Diamond ni miongoni mwa wanamitandao waliomsherehekea Tanasha na mwanawe.
"Bi Ayyksha❤️😍," Mobetto aliandika chini ya chapisho la Tanasha.
Tanasha hakusita kujibu ujumbe wa Mobetto huku akimthibitishia kuwa anampenda.
"Nakupenda🥰," Tanasha alimjibu Mobetto.
Mwanasoshalaiti Huddah Monroe na mwanamuziki kutoka Nigeria Omah Lay ni baadhi ya wanamitandao wengine waliowasherehekea Tanasha na Naseeb Jnr.