'Usimchezee mtoto wa watu,'Romyjons amwambia Diamond huku uvumi wa hurusi yake ukienea

Muhtasari
  • Mitandao ya kijamii imezidi kuwaka moto baada ya uvumi kuenea na kuvuma kwamba staa wa bongo Diamond Platnumz amefunga pingu za maisha
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Mitandao ya kijamii imezidi kuwaka moto baada ya uvumi kuenea na kuvuma kwamba staa wa bongo Diamond Platnumz amefunga pingu za maisha.

Habari hizo zilitangawa na Wasafi Fm huku mama yake akifichua kwamba mwanawe amefunga pingu za maisha.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa nduguye msanii huyo, alimuonya dhidi ya kumchezea msichana wa watu.

Mapema mwezi jana staa huyo wa bongo alikiri kwamba anajua kwamba yeye ni 'player' na kuwa ana mtoto na mwanamke aliyeoolewa.

Pia alisema kwamba hajawahi muona mwanawe kwani haruhusiwi.

Jumbe wake Romy Jons umeibua hisia mitandaoni, huku baadhi ya wanamitandao wakidai kwamba Diamond hawezi kukaa na mwanamke mmoja.

"Mara ya mwisho narudia bwana NASIBUMFUNGE NDOA MWEZI HUU MAANA BARAKA ZAKE ALLAH NDIO ANAZIJUAUSIMCHEZEE MTOTO WA WATU," Romy Aliandika.