logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Inanikwaza sikuwahi kukuambia nakupenda kabla kuaga" Otile Brown amkumbuka marehemu mamake

Otile Brown alimsherehekea mamake kwa kuchangia mafinikio yake makubwa ya sasa.

image
na Samuel Maina

Burudani11 April 2022 - 07:22

Muhtasari


  • •Otile Brown alimsherehekea mzazi huyo wake ambaye aliaga takriban miaka 16 iliyopita kwa kuchangia mafinikio yake makubwa ya sasa.
  • •Baada ya kifo cha mamake, Otile Brown alichukuliwa na nyanya yake ambaye alijaribu kujaza pengo lililoachwa.

Mwanamuziki Jacob Obunga almaarufu Otile Brown alimkumbuka marehemu mama yake wikendi ambayo imetamatika.

Otile Brown alimsherehekea mzazi huyo wake ambaye aliaga takriban miaka 16 iliyopita kwa kuchangia mafinikio yake makubwa ya sasa.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 30 hata hivyo alisema anajuta sana kutowahi pata fursa ya kumwambia mamake jinsi alivyompenda kabla ya kifo chake.

"Marehemu mama. Shukran kwa kunifanya mwanaume niliye sasa. Inanikwaza sikuwahi kukuambia nakupenda kabla kuaga dunia," Otile alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Otile Brown aliambatanisha ujumbe wake na wimbo ambao alitengeneza maalum kwa mzazi huyo wake.

"Inanikwaza sikuwahi kukuambia nakupenda kabla uondoke. Na inanichoma moyo wangu, inaikwaza nafsi yangu maana sikupata muda mama yangu.." Wimbo huo wake ulisema.

Hapo awali Otile Brown aliwahi kufichua kuwa mama yake aliaga dunia mwaka wa 2006. Wakati  huo Brown ambaye ndiye kifunga mimba katika familia yao alikuwa na umri wa miaka 14 tu.

Baada ya kifo cha mamake, Otile Brown alichukuliwa na nyanya yake ambaye alijaribu kujaza pengo lililoachwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved