'Hatujasuluhisha chochote,'Carrol Sonie azungumza baada ya madai ya kurudiana na Mulamwah

Muhtasari
  • Pia amesema kwamba kama mcheshi huyo anataka kusuluhisha mambo yao lazima aombe msamaha mitandaoni
Carol Muthoni katika studio za Radio Jambo
Carol Muthoni katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Dakika chache baada ya mcheshi Mulamwah kupakia viideo akiwa na baby mama wake Sonie na mashabiki kugadhabishwa na kitendo chao huku wengi wakisema ni kiki, kupitia kwenye ukrasa wa Sonie alitoa taarifa na kusema kwamba hawajarudiana na Mulamwah.

Sonie alisema kwamba alikuwa ameenda 'Photoshoot' na wala hakufahamu kwamba atapatana na Mulamwah.

Pia amesema kwamba kama mcheshi huyo anataka kusuluhisha mambo yao lazima aombe msamaha mitandaoni.

"Nilipomuuliza anataka nini hapo aliniambia kwamba anataka kuomba msamaha, nilisisitiza kwamba anapaswa kuomba msamha mitandaoni lakini aliniambia anataka tuongee kwanza."

Hii hapa taarifa yake;