logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sitaki kupata watoto! Bintiye Mike Sonko atangaza

Sandra Mbuvi aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba na hayupo katika harakati za kutafuta.

image
na Samuel Maina

Burudani14 April 2022 - 04:00

Muhtasari


  • •Sandra Mbuvi aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba na hayupo katika harakati za kutafuta.
  • •Kipusa huyo alisema ikiwa angetakiwa kuchagua kati ya pesa na furaha angependa kuishi kwa furaha badala ya utajiri.
Mike Sonko na Bintiye Sandra Mbuvi

Binti wa mwisho kuzaliwa wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko, Sandra Mbuvi almaarufu Thicky Sandra alishirikisha wafuasi wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram.

Katika kipindi hicho, Sandra alizungumzia masuala kadhaa kuhusu maisha yake kama alivyoulizwa na wafuasi wake.

Kipusa huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba na hayupo katika harakati za kutafuta.

"Nipo single na sitafuti.. nataka muda wangu na sihitaji mwanaume," Sandra alijibu mashabiki waliouliza kuhusu hali ya mahusiano yake.

Sandra alipoulizwa kuhusu mipango yake ya siku za usoni aliweka wazi  kwamba hana mipango ya kuwahi kupata watoto.

"Hapana" Sandra alijibu mfuasi aliyeuliza kuhusu mipango yake ya uzazi.

Mfanyibiashara huyo mdogo alisema ikiwa angetakiwa kuchagua kati ya pesa na furaha angependa kuishi kwa furaha badala ya utajiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved