Nimepitia mengi, naskia kupumzika na kubarikiwa-Anerlisa Muigai

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba amepitia mengi, na kwamba kwa sasa anahisi kwamba amebarikiwa
Mrithi wa Keroche, Anerlisa Muigai
Mrithi wa Keroche, Anerlisa Muigai
Image: Instagram

Mfanyibiashara Anerlisa Muigai alifahamika sana mitandaoni baada ya kufunga pingu za maisah ya msanii kutoka Tanzania Ben Pol.

Pia alivuma mitandaoni baada ya kumpoteza dada yake Tecra.

Mama ya Anerlisa alishinda tikiti ya UDA katika uteuzi wa useneta wa Nakuru, huku imlazimu kumwandikia ujumbe wa kipekee.

Baada ya Anerlisa kutalikiana na mumewe, anaonekana kuendelea na maisha yake huku akijitosa kwenye biashara.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba amepitia mengi, na kwamba kwa sasa anahisi kwamba amebarikiwa.

"Siku ya leo ni moja wapo wa siku ambazo naweza sema naskia nimepumzika na kubarikiwa nimepitia mengi, kumpoteza da yangu, talaka,biashara ya familia kuathiriwa na kukabiliana na kuvamiwa," Aliandika Anerlisa.

Aidha Anerlisa amekiri kwamba anajihisi akiwa na amani, na kupendwa.

"Sasa najihisi nina amani, kupendwa na kupata motisha zaidi, kila kitu kinafanyika kwa sababu zake na kwa maombi kila kitu kinafanyika kwa wakati wake kuna mwanagaza mwishoni mwa handaki."