Watu ni wajinga mitandaoni-King Kaka azungumzia uvumi wa kuwa baba ya mtoto wa kijakazi wake

Muhtasari
  • Aliongeza zaidi kwamba  ameishi na meneja wa nyumba yake kwa zaidi ya miaka 8
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Rappa maarufu nchini King Kaka kwa mara ya kwanza amezungumzia uvumi ambao umekuwa uienea mitandaoni kuwa ni baba ya mtoto wa kijakazi wake.

Uvumi huu ulijiri baada ya Nana na Kaka kupakia picha za watoto wao bila ya kumuacha mtoto wa meneja wa nyumba yao.

Akiwa kwenye nahojiano na mpasho Kaka alisema kwamba watu wana ujinga mitandaoni, na wala hajui kwa nini wanawe wanafanana na mtoto wa meneja wa nyumba yake.

Aliongeza zaidi kwamba  ameishi na meneja wa nyumba yake kwa zaidi ya miaka 8.

"Sijui kwanini wanafanana sana. Wamekaa pamoja kwa muda mrefu. Tunavaa sawa... Watu ni wajinga mtandaoni, wanajaribu kusukuma hadithi ambazo hazipo,” rapper huyo alimwambia Mpasho kwenye mahojiano maalum ya kipekee.

King Kaka alisema anamchukulia mtoto huyo na mama yake kama wanafamilia wao.

"Tumekuwa na msimamizi wa nyumba yangu kwa muda mrefu sana tangu binti yangu azaliwe. Zaidi ya miaka 8."