King Kaka afichua alichoambiwa na Mungu baada ya kuzunguma naye moja kwa moja

Muhtasari
  • King Kaka afichua alichoambiwa na Mungu baada ya kuzunguma naye ana kwa ana
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Rappa King Kaka ameweka wazi kuwa amepona ugonjwa ambao ulimfanya alazwe hospitali kwa zaidi ya miezi miwili.

Akiwa kwenye mahojiano na Mpasho Kaka alifichua kwamba wakati huo alizungumza na Mungu ana kwa ana nayachukulia hayo kuwa ni maisha yake ya pili tangu Mungu ampe nafasi ya pili ya kuishi.

Anaongeza kuwa afya yake imeimarika, na amepata uzito mkubwa ambao alipoteza kutokana na maradhi hayo.

“Mimi ni mzima sasa nimeongeza uzito na ningeanza kwenda mazoezini naona hata tumbo limenenepa, ninafuraha kwa awamu hii ya pili ya maisha yangu, Mungu ananionyesha maajabu katika maisha haya ya pili. karibu robo tatu ya mikataba imekuja baada ya maisha yangu ya pili," alisema.

Maisha yake, anasema, yamejaa baraka tangu wakati huo.

"Kuna mpango mwingine uko njiani. Nilikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Mungu, aliniambia niendelee kufanya kile ninachofanya kwamba sababu ya mimi kuwa katika ulimwengu huu ni kutumika," King Kaka alisema.