logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Masomo muhimu unayopaswa kujifunza kutoka kwa hadithi ya msanii Sammy

Hili limezua mjadala baadhi wakidai kwamba anafaa kuachiliwa

image
na Radio Jambo

Habari20 April 2022 - 13:58

Muhtasari


  • Masomo muhimu unayopaswa kujifunza kutoka kwa hadithi ya msanii Sammy
Jail bars

Msanii wa nyimo za kikuyu Sammy aliwaacha wengi na hisia tofauti mitandaoni baada ya kufichua kwama amefungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuiba na vurugu.

Hii ilikuwa ni baada ya rafiki yake kuacha baadhi ya vitu ndani ya nyumba yake vilivyokuwa vimeibiwa. Baadaye aliaga dunia baada ya kuhusika katika ajali.

Hili limezua mjadala baadhi wakidai kwamba anafaa kuachiliwa huku wengine wakikisia kuwa huenda majaji walifanya uchunguzi wao kabla ya kutoa uamuzi huo.

Kutoka kwa hadithi hii, tunajifunza masomo kadhaa.

1.Tunajifunza kujua marafiki zetu ni akina nani kabla ya kuwaingiza kabisa maishani mwetu,Jua wanatoka wapi, chanzo chao cha mapato na uaminifu wake.

2.Licha ya kmatatizo tunapaswa kuomba na kutabasamu kwa matumaini ya kufunguliwa kutoka kwa minyororo ikiwa ni mbaya. Ikiwa ni kweli Sammy hana hatia, tunaomba siku moja aachiliwe. Tunaweza kupatwa na hali zilizo nje ya uwezo wetu lakini zisizidi rasilimali za Mungu.

3.Kila kitu kinatendeka kwa sababu

Iwapo unapitia jambo fulani jua kuwa Mungu alikuwa na sababu yake uoitie jambo hilo, na kuna wakati atadhihirisha kwamba sababu yake haikuwa mbaya.

4.Tuwe na hisia kuhusu familia zetu au jamaa zet wa karibu iwapo tuko kwenye tatizo, watahisi aje na watatusadia vipi ili kutatua matatizo yetu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved