Wacheni watu wakufe wakati wao kwa heshima-Huddah Monroe kwa wanaoeneza uvumi wa uongo

Muhtasari
  • Pia kuna wale wamekabiliana na kejeli nyingi hata baada ya kuthibitisha kwamba uvumi huo ni wa uongo
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Huddah Monroe

Mwanasosholaiti Huddah Monroe ameonekana kuwashambulia na kuwakemea wanamitandao ambao wamekuwa waieneza uvumi wa uongo kuhusu watu wengine.

Kwa kweli mitandao ya kijamii ina mambo mengi, huku kama huyuko makini unaweza kuangukia katika mtego wa uongo.

Kuna baadhi ya watu mashuhuri wamejipata katika upande mbaya wa mitandao ya kijamii, baada ya uvumi wa uongo kuenezwa juu yao.

Pia kuna wale wamekabiliana na kejeli nyingi hata baada ya kuthibitisha kwamba uvumi huo ni wa uongo.

Huddah ameonekana kugadhabishwa na tabia hiyo huku akiwaonya wanamitandao kwamba wanapaswa kuwaacha watu waishi maisha yao.

"Usieneze uvumi ya kuwa mtu ameaga dunia wakati hajaaga dunia, kutopakia kwenye mitandao ya kijamii haimaanishi mtu ameaga dunia aua aishi maisha yake

Sio kila mtu anajishughulisha na mitandao ya kijamii, na wala sio kila mtu anataka kuwa kwenye mtego huu milele,ni mazingira tu yametufanya tuwe kwenye mitandao ya kijamii, bali tukaingia katika mteo huu," Aliandika Huddah.

Yote tisa kumi ni kuwa Huddah aliwaarifu wanamitandao wawache watu waage dunia kwa heshima na wakati wao ukifika.

"Wacheni mambo hayo feki, wacheni watu waage dunia kwa wakati wao na kwa heshima."