'Maneno hayawezi hata kuelezea jinsi ninavyojisikia,'Pascal Tokodi asema baada ya kubarikiwa na mtoto wa kike

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Pascal alisema kwamba maneno hayawezi eleza jinsi anavyohisi
Grace Ekirapa na Pascal Tokodi
Image: Hisani

Muigizaji na msanii Pascal Tokodi na mkewe Grace Ekirapa ni wazazi wapya mjini, baada ya kubarikiwa na mtoto wao wa kike.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Pascal alisema kwamba maneno hayawezi eleza jinsi anavyohisi.

"Maneno hayawezi hata kuelezea jinsi ninavyojisikia kwa sasa, niliwahi kuigiza kama baba katika sinema na vipindi vya Tv, lakini leo hii ni tofauti, leo nimemshika mtoto wetu wa kike mikononi mwangu na kugundua jinsi nilivyobarikiwa.

Nilimwomba Mungu maisha yaliyojaa upendo na furaha na akanitumia familia yangu

Kwa mrembo wangu Neema, kukuona ukiwa mama leo ilikuwa ni furaha kuu maishani mwangu, Tulifanya malaika Asali. I love you from here to Loiyangalani to malakisi and back 😄

Kwa binti yangu mdogo wa kifalme, ninajivunia mambo mengi maishani mwangu, lakini leo, kukushika mikononi mwangu, nikishika kidole chako kidogo, kuwa baba yako, Kushiriki siku ya kuzaliwa na wewe .... nitaongoza orodha milele, nitakuwa hapa kwa ajili yako daima, nitakupenda na kukulinda kwa kila nilichonacho, daima na Milele ♥️," Aliandika Pacal.

Grace Ekirapa kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema;

"Kwa yule mwanaume ambaye sina aleji na uwepo wake kwa @pascaltokodi ❤️❤️ Nilimuomba Mungu zawadi kwa siku yako ya kuzaliwa akanipa kitu hata pesa siwezi kununua😍 Leo unamkaribisha binti mfalme wako duniani kwani yeye ni zawadi Mungu aliamua kukupa kwa siku yako ya kuzaliwa na nina heshima kuwa nimepata bahati ya kumbeba kwa ajili yetu❤️❤️❤️Happy Birthday My Love and Happy Born day to Baby AJ❤️❤️❤️❤️ I love you two soo much."