logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Khaligraph Jones ameahirisha kutoa kibao chake ili kumuomboleza Kibaki

Kwenye wimbo huo amemshirikisha mwimbaji Adasa.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 April 2022 - 12:54

Muhtasari


  • Rapa huyo pia aliungana na Wakenya kumuomboleza Mwai Kibaki kama shujaa wa taifa - kufuatia kifo chake Ijumaa wiki jana
khali-e1471415170725

Rapa Mkenya ambaye ni mshindi wa tuzo nyingi, Khaligraph Jones ameahirisha kutolewa kwa video yake ya muziki iliyokuwa ikitarajiwa ‘Maombi ya Mama’ kwa heshima ya marehemu Rais Mwai Kibaki.

Katika sasisho lililotolewa na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Blue Ink, video inayohusika ilikuwa imeratibiwa kutolewa wiki hii - lakini italazimika kungoja hadi Mkuu wa zamani wa Nchi azikwe.

Rapa huyo pia aliungana na Wakenya kumuomboleza Mwai Kibaki kama shujaa wa taifa - kufuatia kifo chake Ijumaa wiki jana.

Maombi Ya Mama otw, was supposed to drop this week but We had to postpone it to Next week after losing a National Hero (R.i.p Kibaki 🙏🏾) on Wednesday We go Live on YouTube, Meanwhile, Keep on Streaming invisible Currency, Link In Bio #respecttheogs," Aliandika Khaligraps.

Maombi ya Mama ni wimbo nambari 7 kutoka kwa albamu yake ya nyimbo 17 Invisible Currency.

Kwenye wimbo huo amemshirikisha mwimbaji Adasa.

Wengine walioshirikishwa kwenye Albamu ya Papa Jones ni pamoja na; Alikiba, Prince Indah, Mejja, Blackway, Rudeboy, Kev the Topic, Scar, Xenia Manasseh, na Dax.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved