(+Video) "Kifo umepeleka Kibaki wapi?" Embarambamba amwomboleza Kibaki katika wimbo

Muhtasari

•Video ya wimbo huo inaonyesha Embarambamba akisakata densi katika shamba la mahindi, akipanda miti na kujibingirisha matopeni.

Mwanamuziki mashuhuri Christopher Nyangwara Mosioma almaarufu Embarambamba ametoa kibao kipya maalum kwa Hayati Mwai Kibaki.

Embarambamba ambaye anatambulika sana kutokana na mtindo wake tatanishi wa kucheza densi unaohusisha sarakasi nyingi amemwomboleza rais huyo wa zamani katika wimbo huo 'Kibaki'.

Katika wimbo huo, Embarambamba amebainisha kuwa  Wakenya watampeza sana rais huyo wa zamani hasa kutokana na hotuba zake zenye ucheshi.

"Kibaki eeh Kibaki. Kibaki amekufa Kibaki (*2) Kifo, Kifo umechukua Kibaki wapi?" Sehemu ya wimbo wa Embarambamba inasema. 

Msanii huyo kutoka Kisii alimtambua Hayati kwa kuzindua elimu bila malipo, kukuza uchumi na kukubali kugawana serikali na Raila Odinga.

Video ya wimbo huo inaonyesha Embarambamba akisakata densi katika shamba la mahindi, akipanda miti na kujibingirisha matopeni.