Miracle Baby alazwa hospitalini, ahitaji msaada ili kufanyiwa upasuaji

Muhtasari

•Miracle Baby alianza kukumbwa na matatizo kwenye utumbo wake mwakani 2018 na hata kulazimika kufanyiwa upasuaji .

•Miracle Baby anahitaji kufanyiwa upasuaji wa pili hivi karibuni ambao unagharimu shilingi laki tatu.

Miracle Baby
Miracle Baby
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa Gengetone na Mugithi Peter Mwangi almaarufu Miracle Baby amelazwa hospitalini kutokana na matatizo wa tumbo.

Mwanamuziki huyo alianza kukumbwa na matatizo kwenye utumbo wake mwakani 2018 na hata kulazimika kufanyiwa upasuaji .

Kulingana na taarifa iliyotolewa Alhamisi, mwanamuziki huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili  baada ya kuzidiwa na hli yake.

"Mwaka wa 2020, tumbo yake ilianza kuuma mara kwa mar hadi jana (Jumatano)  ambapo ilianza kuuma sana na tukampeleka katika hospitali ya Uhai Neema akiwa amepoteza fahamu,"  Taarifa hiyo ilisoma.

Picha za X-Ray zilibzinisha kuwa tatizo ambalo lilifanya msanii huyo kufanyiwa upasuaji miaka minne iliyopita limerudi.

Miracle Baby anahitaji kufanyiwa upasuaji wa pili hivi karibuni ambao unagharimu shilingi laki tatu.

"Tunaomba msaada wenu marafiki. 0719848841," Taarifa ilisoma.

Mpenzi wake Carol Katrue alipakia video inayoonyesha akiwa amelala katika kitanda cha hospitali na kumtakia afueni ya haraka.

"Afueni ya haraka babe. Najua wewe ni shujaa na utashinda vita hizi. Kila la kheri mpenzi," Alisema kupitia Instagram.

Miracle Baby ni mmoja wa bendi ya Gengetone, Sailors ambayo ilivuma sana miaka michache iliyopita hasa kutokana na kibao 'Wamlambez'