'Sio haki kumkejeli,'Daddy Owen amtetea mjukuu wake Kibaki

Muhtasari
  • Daddy Owen amtetea mjukuu wake Kibaki
  • Daddy Owen aliongeza kuwa mitandao ya kijamii inaweza kuwa nafasi isiyo salama kwa watu wasio na hatia ambao wanahukumiwa kutokana na taarifa zisizo za kweli
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji Daddy Owen amemtetea mjukuu wa marehemu Mwai Kibaki ambaye alishtakiwa kwa kumpuuza Raila Odinga wakati wa mazishi ya rais wa zamani huko Othaya.

Video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha mjukuu wa Kibaki akitazama pembeni wakati Waziri Mkuu huyo wa zamani alipomwendea ili kumsalimia.

Akizungumzia masaibu hayo, Daddy Owen alisema haikuwa haki kumfanyia kijana huyo uonevu kwa sababu ya video iliyohaririwa.

"Nimeona watu wengi wakimnyatia huyu kijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni video sahihi ambayo unaona wazi kuwa kijana huyo anampa mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Raila Odinga, si haki kwamba watu wamemhukumu kutwa nzima ilhali alikuwa akimkwepa mpiga picha huyo na wala si Waziri Mkuu wa zamani,” aliandika kwenye chapisho la mtandao wa kijamii.

Daddy Owen aliongeza kuwa mitandao ya kijamii inaweza kuwa nafasi isiyo salama kwa watu wasio na hatia ambao wanahukumiwa kutokana na taarifa zisizo za kweli.

"Inasikitisha kwamba katika mitaa ya mitandao ya kijamii unaweza kuhukumiwa isivyo haki kwa watu kukimbilia maamuzi."

Jimmy Kibaki akizungumzia video hiyo, alisema kwamba watu wanapaswa kuelewa hisia, haswa wakati huu familia yao inakabiliana na magumu.