Mwanamume hutulia pale anapopata amani,sio urembo-Mejja

Muhtasari
  • Lakini sababu kuu ya uhusiano wa kimapenzi kutodumu katika karne hii ya sasa ni ipi?
Mejja
Image: Hisani

Msanii Mejja ni mwanamuziki ambaye anafahamika sana Afrika Mashariki kutokana na bidi ya kai yake ya usanii.

Mejja ni miongoni mwa wasanii ambao wamesalia katika tasnia ya muiki kwa muda mrefu sasa, huku wakionyesha bidii yao kila siku.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amepakia ujumbe kuhusu wanaume, huku akiamini kwamba mwanamume hukaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kutokana na amani ambayo anapokea.

Pia msanii huyo alisema kwamba sio pesa wala urembo unaomfanya mwanamume kukaa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

"Mwanamume hutulia mahali anapata amani,sio urembo,sio pesa wala sio cheo bali amani," Aliandika Mejja.

Tumewaona wengi wakitangaza uhusiano wao wa kimapenzi mitandaoni huku baada ya muda mchaceh wanaachana,huku wengi wao wakitalikiana kwa jambo moja au nyingine.

Lakini sababu kuu ya uhusiano wa kimapenzi kutodumu katika karne hii ya sasa ni ipi?