logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Tunakupenda" Diana Marua amsherehekea aliyekuwa mpenzi wa Bahati, Yvette Obura

Yvette amemhakikishia Yvette kuhusu upendo mkubwa wa familia yake il kwake.

image
na Samuel Maina

Burudani08 May 2022 - 13:12

Muhtasari


  • •Diana amemtakia mzazi huyo mwenza wa Bahati kheri za siku ya kina mama  na kumtaja kama mtu mwenye roho nzuri.
  • •Yvette Obura pia amemsherehekea Diana pamoja na mama yake na dada yake Mercy Obura.

Huku dunia yote ikiadhimisha siku ya kina mama, mwanavlogu Diana Marua amemsherehekea aliyekuwa mpenzi wa mumewe Yvette Obura.

Diana amemtakia mzazi huyo mwenza wa Bahati kheri za siku ya kina mama  na kumtaja kama mtu mwenye roho nzuri.

"Kheri za siku ya kina mama kwa mtu huyo mwenye roho nzuri Yvette Obura. Unajua mahali ulipo ndani ya mioyo yetu. Tunakupenda," Diana amemwandikia Yvette kupitia Instagram.

Mama huyo wa watoto wawili amemhakikishia Yvette kuhusu upendo mkubwa wa familia yake il kwake.

Yvette ambaye anafahamika zaidi kama Mama Mueni pia amemsherehekea Diana pamoja na mama yake na dada yake Mercy Obura.

"Kheri za siku ya kina mama kwa wanawake hawa wa ajabu. Mama yangu, dada yangu Mercy Obura na Mama Heaven, Diana Marua," Yvette ameandika.

Licha ya kuwa wana wote wawili wamewahi kupata mtoto/watoto na Bahati, wamedhihirisha wazi kuwa hakuna uhasama wowote ulio kati yao kwa sasa.

Hata hivyo wawili hao waliposhiriki mazungumzo hivi majuzi walifichua kuwa hali haijakuwa vile tangu jadi. Walikiri kuwa walitofautiana na kuvurutana miaka ya hapo awali kabla ya kufikia hatua ya kutamatisha ugomvi wao na kushirikiana.

Diana alifichua kuwa ugomvi wake na Yvette ulianza baada yake kupakia picha aliyopigwa pamoja na binti ya Yvette.

"Mimi nilipost picha tu. Wanamitandao walianza kunishambulia wakisema ningemuuliza mamake kwanza. Kulikuwa na mambo mengi. Nilisema uharibifu umeganyika tayari na hakuna kitu ambacho ningeweza kufanya. Nilidhani kitu cha maana kufanya ni kufanya ni kufuta picha lakini Baha alisema nisifute. Hapo ndipo beef ilianza rasmi. Nadhani mimi ndio nilichokoza nyuki," Diana alisema.

Baada ya wawili hao kutofautiana kuhusu suala la picha kulizuka mvutano kati yao kwa muda kabla ya kukubaliana kusuluhisha mizozo yao.

Yvette alifichua alimfikia Diana kupitia mtandao wa Instagram akiomba msamaha kwa yaliyotokea kati yao.

"Nilichukua simu yangu nikakuandikia (Bahati), 'Umekuwa mama mzuri kwa  Mueni kutokana na yale  ambayo huwa ananiambia. Pole kama nimewahi kukosea ama kufanya maisha yako yawe mazuri. Nisamehe na ningetaka tuwe mahali pazuri'. Kusema kweli sikudhani ungejibu," Yvette alimwambia Diana.

Wawili hao walifichua walilazimika kushirikiana katika malezi ya Mueni baada ya Bahati kuwaagiza wawe wanawasiliana.

Licha ya yote Diana aliweka wazi kuwa Yvette hakuwahi kumkosea heshima licha ya kuwa kulikuwa na ugomvi kati yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved