Nitakukumbuka daima,'Msanii Ben Cyco amuomboleza dada yake

Muhtasari
  • Huku akimuomboleza dada yake kwenye ukurasa wake wa instagram, Ben alisema kwamba atampenda na kumkumbuka dada yake kila wakati

Kumpoteza mpendwa wako haswa mzazi,ndugu au dada ni jambo ambalo linauma sana maishani.

Kifo ni jambo ambalo haliwezi kuepukika.

Ni takriban miaka 2 baada ya msanii wa nyimbo za injili Ben Cyco ampoteze dada yake, ambaye alikuwa anaugua saratani.

Huku akimuomboleza dada yake kwenye ukurasa wake wa instagram, Ben alisema kwamba atampenda na kumkumbuka dada yake kila wakati.

"Ni miaka 2 leo tangu utuache, endelea kupumzika dada yangu nitakupenda na kukukumbuka daima @fu.raha , daima ❤️,"Ben Aliandika.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki;

milliekigs: Her memories live on. Remembering her warms our hearts today as she always did. Continue resting eazy Joy. ❤️

deliberateconscious_movement: May her beautiful soul continue resting in Glory 🕊️and may your hearts always find peace in the Truth of God's word🙏

dennohjabali🫂 : May she continue resting in peace eterna

waithira_njagi: Hugs Ben❤️❤️ and time does move fast! Damn!😢

i.t.s.a.r.c.h.i.e: May her beautiful soul continue resting... And may God continue healing your hearts❤️