'Nilipata mapenzi ya kweli,'Jacque Maribe asherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe

Muhtasari
  • Jacque Maribe asherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe
  • Pia Maribe akimsherehekea mwanawe amesema kwamba baada ya kumpata mwanawe alipata mapenzi ya ukweli
Jacque Maribe na mwanawe
Image: Hisani

Ni furaha ya kila mama kumuona mwanawe au wanawe wakikua kila siku, na kukua kutoka kiwango kimoja hadi kingine.

Hawakukosea kusema kwamba watoto ni baraka kwa kila mtu, ila kuna wale wana tabia ya kuavya mimba ili waweze kuonekana wazuri.

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe, huku akisherehekea siku ya kuzaliwa na mwanawe amesimulia jinsi, mwanawe aliweza kubadilisha maisha yake.

Pia Maribe akimsherehekea mwanawe amesema kwamba baada ya kumpata mwanawe alipata mapenzi ya ukweli.

Mwanawe Jacque, na mcheshi Eric Omondi Zahari anaadhimisha miaka 8 hii leo.

"Miaka 8 iliyopita leo, maisha yangu kama nilijua yalibadilika kabisa, na kuwa bora. Kichwa kipya, nilipata upendo wa kweli, nilipata kusudi na maana. Nikawa mama, mara mama Zahari. Na nimeipenda kila dakika ya safari hii.

Zahari - maana yake Mungu Amekumbuka. Nisingeweza kukuchagulia jina bora mwanangu. Na kupitia safari yetu, Mungu amekumbuka kwa uaminifu.

Nakupenda kuliko maneno yote katika vitabu vyote katika ulimwengu mzima.

Heri ya miaka 8 ya kuzaliwa, King Zee!!,"Aliandika Jacque.