Staa wa bongo Diamond Platnumz na msanii mwenzake Zuchu wamekuwa gumzo mitandaoni kwa muda sasa.
Hii ni baada ya fununu kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi, uvumi ambao Zuchu aikana na kusema kwamba Diamond anamfahamu mpenzi wake.
Zuchu amekuwa akipakia jumbe huku akimsifia bosi wake na kuzua hisia tofauti kati ya wanamitandao.
ikendi iliyopita wawili hao walizua gumzo mitandaoni baada ya Diamond kumpakata Zuchu kwa njia ya kipekee huku wakiwatumbuiza mashabiki wao kwa kibao chao cha 'mtasubiri'.
Siku ya JUmatatu Zuchu aliwafurahisha mashabiki baada ya kumwambia Diamond kwamba anapomuona anahisi kubarikiwa.
Wengi walitamani kkwamba uhusiano wao na bosi wao ungekuwa kama ule wa Zuchu na Diamond.
"Ninapokuona,ninahisi kubarikiwa," Zuchu alimwambia Diamond.