Hisia kali baada ya Rayvanny kufichua sababu ya kuchoma nyumba yake baada ya kuijenga

Muhtasari
  • Kulingana na msanii huyo hii ni moja wapo ya video ambazo ametumia pesa nyingi kwalo kwa sababu ya ubunif
Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Next level Music, Rayvanny
Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Next level Music, Rayvanny
Image: instagram

Rayvanny amewafanya watu kuzungumza kwenye mitandao tofauti ya kijamii. Hii ni baada ya hatimaye kufichua sababu iliyomfanya kuchoma nyumba yake saa chache baada ya kuijenga.

Kwa mujibu wa Rayvanny, mwimbaji huyo alichoma nyumba wakati wa upigaji picha za video kwa ajili ya ubunifu tu, jambo ambalo limezua tafrani mtandaoni.

Kumbuka Rayvanny si mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Mashariki ambaye anatumia fedha nyingi kwa ajili ya ubunifu katika video.

Tuna watu kama Diamond Platnumuz kuwataja lakini wachache tu, ambao pia wametumia pesa nyingi kwa ajili ya ubunifu.

Sasa habari hii kuhusu Rayvanny kuchoma nyumba kwa ajili ya ubunifu imeenea mtandaoni ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

Wengi wanadai kuwa Rayvanny anaiga kutoka kwa Wanamuziki wa kimataifa huku wengine wakijiuliza inakuwaje mtu ajenge nyumba na kuichoma kwa wakati mmoja.

Kulingana na msanii huyo hii ni moja wapo ya video ambazo ametumia pesa nyingi kwalo kwa sababu ya ubunifu