logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu tattoo 5 maalum zilizochorwa kwenye mwili wa Harmonize

Baadhi ya tattoo zake ni michoro huku zingine zikiwa maandishi.

image
na Samuel Maina

Burudani25 December 2022 - 06:24

Muhtasari


  • •Harmonize amechorwa tattoo zaidi ya kumi kwenye mikono, miguu, shingo, kifua, mgongo na kiuno chake.
  • •Mwaka jana Harmonize alichorwa tattoo ya sura ya rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, John Pombe Magufuli.

Mwanamuziki wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ni miongoni mwa wasanii ambao wamechorwa tattoo nyingi kwenye mwili wao.

Harmonize amechorwa tattoo zaidi ya kumi kwenye mikono, miguu, shingo, kifua, mgongo na kiuno chake. Baadhi ya tattoo zake ni michoro huku zingine zikiwa maandishi.

Tattoo nyingi za bosi huyo wa Konde Music World huwa na maana zake tofauti huku baadhi zikiwa za kusherehekea watu maalum katika maisha yake.

Katika makala haya tutaangazia baadhi ya tattoo za msanii huyo na maana yake;-

1. Tattoo ya Diamond

Miaka kadhaa iliyopita Harmonize alichorwa sura ya aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz kwenye kifundo cha mkono wake kushoto.

Mwaka jana mwanamuziki huyo alithibitisha kuwa tattoo hiyo bado ipo licha ya uhasama mkubwa uliopo kati yao.

"Licha ya yote, mimi nina heshima kubwa kwake. Leo hii licha ya makelele yote unayosikia niko na tatoo ya Diamond. Hii ni sura yake. Licha ya yote!" Harmonize alisema.

Konde Boy alisema alipokuwa anachora tattoo ile alitaka iwe kumbukumbu kuwa Diamond alimuinua kutoka sehemu moja hadi nyingine.

2. Tattoo ya jina lake

Mwanamuziki huyo kutoka eneo la Mtwara amechorwa tattoo ya jina lake la utani "Konde Boy" kwenye mkono wake wa kulia.

Tattoo hiyo ni maalum kwake kwa kuwa ni ishara ya kujipenda.

3. Tattoo ya Sarah Michelloti

Mwaka wa 2019 Harmonize alichora tattoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelloti kwenye mkono wake.

Mwanamuziki huyo alipiga hatua hiyo wakati penzi lake na Sarah lilikuwa limenoga  kama ishara ya kumsherehekea kipusa huyo.

Wawili hao hata hivo walitengana baada ya Harmonize kufichua habari kuhusu mtoto ambaye alipata nje ya ndoa.

4. Tattoo ya Kajala na bintiye

Mapema mwaka huu, hatua ya Harmonize kuchorwa tattoo ya aliyekuwa mchumba wake Fridah Kajala Masanja imekuwa gumzo kubwa mitandaoni.

Jambo hili lilifichuka baada ya mwanamuziki huyo kupakia video iliyoonyesha tattoo ya sura ya muigizaji huyo akiwa amemshika binti yake Paula.

Harmonize alipiga hatua hiyo kama mojawapo ya njia ya kumtongoza Kajala ili warudiane  tena baada ya kuwa wamekosana mwaka jana.

5. Tattoo ya Magufuli

Mwaka jana Harmonize alichorwa tattoo ya sura ya rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, John Pombe Magufuli.

Harmonize alichorwa tattoo hiyo baada ya hayati kufariki kama hatua ya kusherehekea maisha yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved