Msanii Diana Marua almaarufu Diana B akiwa kwenye onyesho lake la upishi, alimualika msanii Stivo Simple Boy kuwa na gumzo naye.
Ni wazi kwamba msanii huyo amekuwa gumzo mitanddaoni baada ya kuachana na ampenzi wake Pritty Vishy huku wawili hao wakirushiana vijembe.
Diana na Stivo walikuwa wanapika chapati, katika kipindii hicho ambacho Diana hualika wasanii na watu mashuhuri tofauti.
Huku wakiendelea na shughuli zao Stivo alianza kumrushia Diana mistari na kusifia urembo wake.
Stivo alimwambia Marua kwamba anataka awe mke wake kutokana na maumbile yake,
"Mwili wako uko sambamba, hauna gongingo na ningependa uwe mke wangu. Je inawezekana," Stivo aliuliza.
Diana alisalia bila usemi wowote huku Stivo akisubiri majibu ya Diana Marua.