'Nimebarikiwa sana kushiriki maisha na wewe,'Joyce Omondi amsherehekea mumewe

Muhtasari
  • Joyce alimtaja Waihiga kama mwanaume aliyekusudiwa kwake akisema kwamba amebarikiwa kushiriki maisha naye

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mtangazaji wa runinga ya Citizen  Joyce Omondi ameandika ujumbe wa kufurahisha kwa mumewe Waihiga Mwaura anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Joyce alimtaja Waihiga kama mwanaume aliyekusudiwa kwake akisema kwamba amebarikiwa kushiriki maisha naye.

"Heri ya siku ya kuzaliwa kwa mwanamume wa ndoto zangu na mpenzi wa maisha yangu, #theoneHekeptforme @waihigamwaura ❤️❤️❤️Nimebarikiwa sana kushiriki maisha na wewe. Asante kwa wewe ni nani na yote unayofanya

Hakika wewe ni zawadi inayostahili kusherehekewa kila siku. Kwa hivyo hapa kuna miaka mingi zaidi iliyojaa furaha, upendo, neema na kila kitu kizuri kutoka juu!'' Bi.Omondi aliandika.

Mnamo Desemba 31, mtangazahi huyo alikiri kwamba mwaka wake wa 2021 ulikuwa wa machozi na huzuni nyingi. Alimpoteza babake mnamo Juni, 2021.

"Kusema ukweli, nilitumia muda mwingi wa 2021 nikilia na kuvunjika moyo. Lakini mwaka unapoisha, moyo wangu unajawa na shukurani kwa sababu najua kuwa nimesimama hapa kwa sababu ya neema ya Mungu tu 💯.