Iliniuma-Otile Brown ataja sababu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nabii

Muhtasari
  • Otile Brown ataja sababu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nabii
Image: INSTAGRAM// OTILE BROWN

Tangu kuachana na Nabii, Otile Brown amekuwa kimya sana na tumekuwa tukimuona peke yake, akiachia nyimbo na kutofanya mahojiano yoyote na wanablogu au hata Vituo vya Tv miezi 6 iliyopita.

Mtangazaji Ali alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Otile Brown na akamuuliza kuhusu kuachana kwake na Nabii.

Otile Brown alisema kuwa haikuepukika kwa sababu ya masuala kadhaa ambayo yanaeleweka.

Jambo la kwanza, Nabii hakuwa tayari kuhamia Kenya kwa sababu ya baadhi ya masuala ya kifamilia ambayo yalikuwa muhimu sana katika tamaduni za Waethiopia, jambo lingine lilikuwa ni kuhusu baadhi ya mambo ambayo yalitaka awe nje ya Kenya.

Uhusiano wa umbali mrefu haukufaulu na kwa sababu zisizoweza kuepukika wakati mwingine Nabii angeweza kuchukua muda mrefu sana kurejea Kenya.

Otile alisema kuwa wote wawili walikubali na kuamua kuachana, na labda ikiwa imepangwa wao kuoana, inaweza kutokea siku zijazo.

Huku akizungumzia ugomvi wake na  Arrow Bwoy miezi michache iliyopita, Otile alisema kuwa Arrow alitoa kolabo hiyo bila ridhaa yake - akielezea hatua hiyo kama isiyojali na isiyo ya kitaalamu.

"Tulikuwa tumezungumza na Arrow Bwoy ni miongoni mwa wasanii niliowaheshimu sana. Ninawaheshimu nyote na ninamuogopa Mungu sana," Otile alisema.

"Arrow Bwoy aliniuliza kama tunaweza kutoa wimbo huo na nikasema hatuwezi kuutoa kwa vile wimbo huo ulikuwa wa zamani lakini akaendelea na kuutoa."