Wakenya hawajapata vya kutosha kuhusu drama ya Akothee na mpenzi wake Nelly Oaks. Baada ya kummwagia sifa kemkem na kuahidi hata kumpa watoto, hatimaye Akothee aliachana na Nelly Oaks.
Alipoulizwa kuhusu hilo Akothee alithibitisha kutengana na kuahidi kutochumbiana tena.
Pia alisema kuwa hayuko tayari kulizungumzia au kujibu maswali yoyote kulihusu.
Jana Akothee alitumia ukurasa wake wa Instagram kufichua kile ambacho uchumba umekuwa ukimfanyia.Alisema alipokuwa kwenye uhusiano alikuwa akilazwa hospitalini kila mara.
Huu ni mwaka wa 2017,2018 na 2019.
Mnamo 2020 alipoamua kusalia peke yake hakuwahi kwenda hospitalini na hakuwahi kunywa dawa yoyote ikiwemo Panadol. Alikuwa na amani mwaka huo.
Mnamo 2021 Juni alipendana na Nelly Oaks. Miezi mitatu chini ya mstari huo, alilazwa hospitalini tena na mbali na hayo alikuwa na msono wa mawazo kwa zaidi ya miezi 6. Aliapa hatawahi kuchumbiana tena.