Wanamitandao wamtakia Simon Kabu afueni ya haraka baada ya kulzawa hospitali

Muhtasari
  • Wanamitandao wamtakia Simon Kabu afueni ya haraka baada ya kulzawa hospitali
Sarah Kabu na Simon Kabu
Sarah Kabu na Simon Kabu
Image: HISANI

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Bonifire Simon Kabu anaendelea kupata afueni baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Jumanne.

Habari za ugonjwa wake zilitangazwa na mkewe Saraha Kabu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram.

Saraha akufichua alichokuwa anaugua mumewe, bali aliwataka mashabiki wamtakie afueni ya haraka.

"Hapa ndipo unapoelewa kwanini iliwabidi kujumuisha KATIKA UGONJWA NA AFYA KWA NADHIRI ZA NDOA. Unapomsindikiza mwenzi wako anapoenda theatre halafu anakuomba busu la kwaheri 💋 kabla hajatuliza basi unakumbuka wimbo wa @evans_demathew 🎵 akijira uka ngumumunye... 😭😭wah jana ilikuwa ni siku ya hisia hasa ile 1hr alikuwa ndani ya theatre. ila tunamshukuru Mungu kwa utaratibu uliendelea vizuri 🙏 ungana nami kumtakia mume wangu @kabusimon apone haraka 🙏 ❤️,"Aliandika Sarah.

Haya yanajiri baada ya wawili hao kuanika ugomvi wao mitandaoni miezi chache iliyopita, huku wakirudiana baada ya muda mfupi.