Mastaa wa bongo Baba Levo na Mwijaku wamewashangaza wengi baada ya kufichua kuwa hawajasafiri hata siku moja kutoka ardhi ya Tanzania kuenda kutumbuiza mashibiki wao nje ya ya nchi hiyo.
Shoo zao nyingi zimekuwa ndani ya mpaka wa Tanzania, ambapo wana mashabiki wengi.
Mwanamuziki Baba Levo aliyaweka haya wazi wakati alikuwa akihojiwa kwenye runinga ya Bongo 5.
''Hatujatoka nje yaTanzania kuperfom ukweli usemwe, baadhi za tamasha zetu ni za hapa nchini Tanzania'' Baba Levo alisema.
Wasanii hawa wawili walipoteza matumaini ya kutumbuiza nje ya Tanzania wakati walipanga safari ya kuenda Uturuki kutumbuiza mashabiki wao lakini safari hiyo ikasitishwa ghafla.
Baba Levo,@officialbabalevo alielezea kuwa @mwijaku ndiye alisababisha safari yao kukatwa walipofika Uwanja wa Ndege.
''Kwa Visa yetu iliandikwa tusafiri tarehe moja mwezi wa saba, jambo ambalo Mwijaku hakutilia maanani kuangalia tarehe vizuri kwa hivyo hatukusafiri'' Alisema Baba Levo.
Kando na kuimba,Baba Levo ni mcheshi pia. Ameshiriki katika kipindi cha Amplifier Countdown cha CloudsFM ambapo alizungumzia wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mwijaku naye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio kutoka Tanzania. Mwijaku anadaiwa kuwa hater maarufu wa Diamond Platinums na WCB kwani mara nyingi huwa anamkashifu.
Msanii Baba Levo ametunga nyimbo kadha zilizomweka katika upeo wa taaluma ya muziki.
Baadhi za ngoma zake zinazofanya tamba ni pamoja na Kanyaga Twende, Vuvuzela miongoni mwa zingine.
Huku Mwijaku anafahamika kwa kibao chake Maramia, ambacho kiliteka anga ya muziki katika Bongo Fleva.