Nataka mpenzi sio 'hotspot'-Ujumbe wa Jimal Roho Safi uliozua gumzo mitandaoni

Muhtasari
  • Jimal amesema kwa sasa anahitaji mpenzi na sio Hotspot maana yake ni mtu anayeweza kushirikishwa na kila mtu
Jimal Rohosafi
Image: Instagram

Mmoja wa wajasiriamali maarufu nchini Kenya na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Amberay, Jimal Rohosafi amezua tafrani mtandaoni baada ya kuandika ujumbe wa Kichefuchefu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kulingana na baadhi ya mashabiki ujumbe huo unaelekezwa kwa aliyekuwa mpenzi wake Amberay.

Tangu kuachana na Amberay, Jimal Rohosafi hajawahi kuendelea, huku kwa upande mwingine Amberay ameshaachumbiana na wanaume zaidi ya 4 na kwa sasa anachumbiana na Rapudo ambaye pia ni mmoja wa wajasiriamali matajiri jijini.

Jimal amesema kwa sasa anahitaji mpenzi na sio Hotspot maana yake ni mtu anayeweza kushirikishwa na kila mtu.

"Ninapogundua kwamna unaumiwa na atu wengi, huwa nakuacha na unaendelea na wao, nataka penzi na wala sio Hotspot," Jimal Aliandika.