Mimi ni mnoma kwa kufoka mstaari kushinda Femi One-Winne Odinga

Muhtasari

•Winnie alikuwa akiwataja wasanii maarufu wa kufoka wakati alipomtambua Femio One kama nyota katika mchezo huo.

•Binti wa Azimio Raila Odinga Winnie amempinga malkia wa muziki wa rap Femi One  kufoka mistari.

Winnie Odinga
Winnie Odinga

Binti wa Azimio Raila Odinga Winnie amempinga malkia wa muziki wa rap Femi One  kufoka mistari.

Katika mahojiano na Mwafreeka Mwaf kwenye podikasti yake ya YouTube, mwanaharakati huyo wa kisiasa alisema anaweza kumshinda Femi One katika  kufoka mistari.

Winnie alikuwa akiwataja wasanii maarufu wa kufoka wakati alipomtambua Femio One kama nyota katika mchezo huo.

“Namchallenge kwa mashindano ya kufoka ,si unajua kenye naweza fanya,ingawa yeye ni mmoja wa marapa ninaowapenda ,lakini mimi bado ni mnoma" Winnie alisema.

Aliwataja Jay Z na Drake kuwa ni marapa anayewafuatilia kimataifa wakati ndani ya nchi, alisema Mbogi Genje, Khaligraph, Mbithi na Wakadinali.

"Napenda Jay Z, Drake, wale watuhumiwa wa kawaida," alisema.

''Hapa Kenya nampenda Mbogi Genje, Wakadinali, kisha rapa mwingine Kamba boy anaitwa Mbithi, halafu kuna binti mwingine anaitwa Roza,” alisema.

Winnie alikiri kuwa Femi One ni mmoja wa wasanii wa muziki wa rap nchini.

Alisema  kuwa ako tayari kwa mashindano na Femi one  kufoka mistari , akionyesha kujiamini na kuwa anawezakumshinda.

Wakati mwingine akifanyiwa mahojiano, Winnie alifunguka kuhusu kwenda katika shule moja ya kifahari na hayati mwanamuziki  wa rap Issah Mmari Wangui almaarufu E-Sir.

Kulingana na Winnie, alijiunga na shule hiyo wakati rapper huyo alikuwa tayari ameondoka lakini mafanikio yake yalikuwa yameandikwa kila mahali.

"E-Sir alikuwa shule ya Brookhouse na alikuwa maarufu zaidi shuleni. Alikuwa mkubwa kuliko mimi, nilijiunga na shule hiyo  mwaka aliondoka. Lakini ulipofika shule, uwepo wa E-Sir ulikuwa kila mahali, alikuwa mwanafunzi bora tuzo baada ya tuzo na sio tu katika muziki lakini pia katika Hisabati ,sayansi utapata E-Sir hapo," Winnie alisema.