Vera Sidika afichua mambo 2 yanayomfanya awape watu block mtandaoni

Muhtasari
  • Vera Sidika afichua mambo 2 yanayomfanya awape watu block mtandaoni

Mwanasosholaiti na mama wa mtoto mmoja, Vera Sidika amefichua vigezo anavyotumia anapowapa block wafuasi kutoka kwenye mitandao yake ya kijamii.

Akimjibu shabiki ambaye alikuwa anataka kujua kuhusu watu ambao amewapa block  kwenye ukurasa wake wa Instagram, Vera alifichua kuwa hawapi block wafuasi bila sababu.

"Wewe njoo kwa DM yangu ukiandika paragraphs of bullsh*t while i mind my business, sitakujibu. Utakula block roho safi.

"Unachukia moja kwa moja bila sababu, nitakupa block ili kukuokoa nishati. Labda kupata ukurasa wangu kunazua chuki. Kwa hivyo nitakuepushia shidakwa kukupa block," Vera Alisema.

"Kinachoshangaza ni kwamba bado watafungua akaunti ghushi ili kutazama kila hatua huku wakizunguka wakiwa watoto wachanga wanaolia na wamezuiliwa," alisema.

Jibu linakuja wakati Corazon Kwamboka na rapa Noti Flow wote walithibitisha kuwa Vera amewapa block  kwenye Instagram.

“Nimekutana naye takribani miaka sita iliyopita lakini hatuingiliani, huwa siangaliiukurasa wa Instagram wa Vera Sidika, kwa sababu fulani nimepewa block... "Nimejua kwa miaka kuwa ameniblock," Alizsema Corazon akiw kwenye mhojiano.