Staa wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya @kingsmusicrecords @officialalikiba ametangaza rasmi tour yake ya nchini Marekani.
Akieleza kwenye Instagram yake @officialalikiba ameeleza kuwa huu ni mwaka wa nne hajawahi kufanya show Marekani hivyo hiyo inaonyesha ni namna gani ame miss kufanya show katika yaifa hilo.
Ameongeza kuwa Tour hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya album yake ya Only one King.
''Siwezi kusubiri kusherekea nanyi tena mashabiki wangu wapendwa'' Alikiba alisema.
Mwimbaji huyo alisema kuwa ziara hiyo itaanza Septemba mwaka huu na tarehe rasmi ya ziara hiyo itatangazwa hivi karibuni.
Tukio kama hii lilionwa kwa Diamond na Harmonize ambao walishafanya ziara yao Marekani, sasa imekuwa kama desturi Wasanii kutoka Bongo kufanya ziara hizo mara kwa mara Merekani.
Wengi wamedai kuwa ziara ya Alikiba Merekani ni kama chanzo cha kujipima ubabe wake huko Merekani kama walivyoshafanya Diamond na Harmonize.
Alikiba Mwaka huu anatazamiwa kufanya makubwa sana katika usani wake huko Marekani kulingana na maandalizi yake mazuri yanayoonekana wazi.
Baadhi ya mashabiki wake kutoka Bongo walifurahishwa na uamuzi wa Alikiba kuzuru Marekani na kuwakilisha muziki wakibongo duniani.
Msanii huyo kando na kuimba, ako na tarjiba ya juu katika kucheza soka, haya yamedhihirika wazi katika baaddhi za mchwano ambazo ameshiriki na timu yake kuibuka mshindi.