Hisia mseto baada ya Omosh kuonekana kwenye uzinduzi wa Manifesto ya Wajackoyah

Muhtasari
  • Hisia mseto baada ya Omosh kuonekana kwenye uzinduzi wa Manifesto ya Wajackoyah
Image: WILFRED NYANGARESI

Mwigizaji  maarufu Joseph Kinuthia almaarufu Omosh amevutia hisia za wengi baada ya kuonekana wakati wa uzinduzi wa manifesto ya Roots Party of Kenya mnamo Alhamisi Juni 30.

Omosh alikuwa amevalia shati jeupe liliyochorwa picha ya Wajackoyah na kauli mbiu 'Uhuru Unakuja.'

Mwigizaji Omosh
Image: WILFRED NYANGARESI

Muigizaji huyo wa zamani wa Tahidi High hapo awali aliahidi utiifu kwa chama cha William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) lakini uwepo wake katika manifesto ya Wajackoyah iliyozinduliwa ulionekana kufichua kuwa Omosh alikuwa amebadili upande wake.

Picha zake akiwa na rangi za UDA na rangi za Roots Party of Kenya zimezua hisia tofauti kutoka kwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii.

Haya yanijiri mieezi chache baada ya mwigizaji huyo kutangaza rasmi kwamba amejiunga na chama cha UDA.kinachoongozwa na naibu rais William Ruto.

Image: WILFRED NYANGARESI