Yamotoband Kuungana tena ?

Watu wengi wamependekeza wao kufanya kazi tena

Muhtasari

•Staa wa Bongo Mbosso akihojiwa na  runinga ya  Wasafi alidokeza kuwa Beka ambaye alikuwa mmoja ya  wasanii ndani ya Yamotoband alikuwa na nia ya kurejesha  Bendi hiyo.

•Mbosso alidai kuwa kuitwa kwake na Beka kushiriki kwa kutoa wimbo, ilikuwa juhudi zake  kuwaleta pamoja tena.

 

Yamotoband
Yamotoband
Image: SCREENGRAB

Staa wa Bongo Mbosso akihojiwa na  runinga ya  Wasafi alidokeza kuwa Beka ambaye alikuwa mmoja ya  wasanii ndani ya Yamotoband alikuwa na nia ya kurejesha  Bendi hiyo.

''Tuliongea na Beka akaniambia kuwa kuna wimbo inafaa tufanye kwa pamoja mimi na yeye, kumbe nia yake ilikuwa ni kutuleta pamoja kama Yamotoband ,ingawa hakuiweka wazi, nikamwambia sawa, na akanitumia wimbo'' Mbosso alisema.

Mbosso alidai kuwa kuitwa kwake na Beka kushiriki kwa kutoa wimbo, ilikuwa juhudi zake  kuwaleta pamoja tena.

''Kwa upande wake aliona hiyo ni njia rahisi  kwake ya kutupata wote, labda kwa wengine pia alifanya hivyo hivyo, juu nimeangalia kwenye utambulisho wake wengine wote pia hawajaenda'' Mbosso alisema.

Staa huyo,pia alidokeza kuwa watu wengi wamependekeza wao kufanya kazi tena ata kama ni kwa mara moja alafu kila mmoja arudi katika shughuli zake za kibinafsi.

''Angeniambia kuwa hii wimbo inafaa tufanye ya Yamotoband mimi ningekubali kwa haraka sana, juu tangu mwaka jana mimi ndo nilitoa hiyo wazo ya kufanya wimbo kwa pamoja tena ,Mimi niliwapigia simu wote nikawaambia inafaa tufanye ngoma ya Yomotoband itatusadia pakubwa'' Mbosso alisema.

Yamotoband inajumuisha wasanii wanne wa Kitanzania wenye vipaji; Dogo Aslay, Maromboso, Enock Bella na Beka.

Hapo awali jina la asili la bendi hiyo ya vijana ilikuwa ni ‘Mkubwa na Wanawe’, lakini baadaye walichukua jina la wimbo wao wa kwanza ‘Yamoto’ ambao ulivuma sana nchini Tanzania.

Yamotoband ilikuwa miongoni mwa kundi la muziki lililosherehekewa zaidi nchini Tanzania, Bendi hiyo ilitawala hewani kwa vibao kama vile ‘Cheza Kwa Madoido’ miongoni mwa vingine.

Mnamo mwaka wa 2017, bendi hiyo ilisabaratika baada ya wasanii kadhaa kuamua kuanza kazi za solo.

Maromboso libadilisha jina na kuitwa Mbosso na kunaswa na Wasafi chini ya Diamond Platnumz.

Inadai kuwa Mbosso labda  ndiye msanii wa solo aliyefanikiwa zaidi kutoka kwa kundi hiyo chini ya mbawa za Diamond.

Mbosso amekuwa akiachia muziki mpya kikamilifu, wimbo wake wa hivi punde zaidi ni Moyo, uliotolewa wiki mbili zilizopita.