Miezi chache baada ya kuwa nambari nne, kwa wafuasi wanaosikizwa kwenye spotify nchini Tanzani msanii Loui amemshirikisha msanii kutoka Ghana Kidi na Maud Elka kwenye kibao chake cha Hennessy.
Wasanii wengine walioongoza katika kuwa na wafuasi wengi kwenye spotify ni pamoja na staa wa bongo Diamond Platnumz,Rayvanny na Harmonize.
Msanii Kidi alifahamika sana kupitia kwenye kibao chake cha 'touch it'.
Kushirikishwa kwake Hidi na Maud kwenye kibao hicho kunaleta mdundo mwingine unaowawezesha mashabiki wake kufurahia kibao hicho.
Kibao chake Loui kimezalishwa na S2kizzy, huku video yake ikiwa imefanyika Tanzania Dar Es Salaam, na kuelekezwa na Director Kenny.
Huku akizungumzia kibao hicho Loui alisema kwamba ni mradi ambao alikuwa ameusuburi kwa muda.
Pia aliwashukuru wasanii hao wawili kwa kujitolea kwao, na kwa msaada wao.
"Nimekuwa nikitarajia toleo hili kwa furaha msisimko, sote tumeweka kazi nyingi, wakati, na bidii katika mradi huu na natumai utakupa kila sababu ya kufurahia na kucheza tena wimbo huu katika msimu wa kiangazi. Nampongeza KIDI na Maud Elka kwa msaada wao juu ya hili, mradi huu haungewezekana bila ubunifu wao mchango na kujitolea”.
Hii hapa video ya kibao hicho;