Mwanamuziki wa kuchana mistari na ambaye pia anajiongeza kama mwanablogu wa YouTube, Diana Marua amefichua kwamba hakuwa kabisa ametarajia ujauzito wa mtoto wake wa tatu ambao pamoja na mumewe walitangaza mapema wiki iliyopita.
Kupitia video ambayo alipakia kwenye YouTube yake, Marua alisema kwamba mnamo mwisho wa mwezi Februari mwaka huu alikuwa anatarajia hedhi yake lakini haikuja na hapo akaingiwa na shauku kwamba huenda amepata ujauzito.
Alisema kwamba hilo tukio lilimshtua mpaka akampigia daktari wa masuala ya kike na kumjulisha suala hio ambapo daktari alimwambia henda ni ujauzito na kumtaka achukue vipimo.
Kulingana na maam huyo wa watoto wawili, hakuwa kabisa anatarajia kupata mtoto wa tatu hivi karibuni ila hilo likatokea.
Msanii huyo alisema kwamba sasa tatizo kubwa linalomkumba sasa hivi ni kutafuta jina la mtoto wake wa tatu baada ya wale wa kwanza wawili Heaven na Majesty.
“Baada ya Heaven na Majesty, wasiwasi wangu mkubwa sasa hivi ni kumpa mtoto wangu wa tatu jina. Siku kwa wakati .... Ninafurahia kila kidogo hatua. Asante kwa maoni yenu yote kwenye Ufunuo wetu. Tunawapenda sana,” aliandika kwenye instagram yake Diana Marua.
Wiki iliyopita wachumba hao walitangaza kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu baada ya ujauzito kuonekana.
Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita Diana Marua aliwahi dokeza kwamba mayai yake yalikuwa yanaanza kumsumbua na ni kama alikuwa anataka mtoto mwingine.
Bahati kwa sasa anang'ang'ana kweney kampeni za kisiasa huku akinuia kuwa mbunge wa Mathare katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 kupitia tikiti ya chama cha Jubilee licha ya visingiti vingi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa muungano wa Azimio One Kenya wanaomtaka kujiondoa na kumuunga mbunge wa sasa mkono.
Hongera kwao!