Mkuza maudhui wa YouTube Thee Pluto amejipata katika majibizano makali na mmoja wa mashabiki wake aliyetaka kujua ni lini mara ya mwisho alikuwa na mtoko na mpenzi wake Felicity Shiru.
Akionesha kwenye instastory za moja ya kurasa zake za Instagram, Pluto aliandika kwamab aliamka na kupata ujumbe huo mrefu kwenye akaunti yake mtu asiyemjua akimkemea kwamab muda wote anashinda mitandaoni kusifia gari lake lakini hajawahi kuwa na muda wa kujivinjari na mpenzi wake Shiru.
“Mara ya mwisho ulimchukua Fel lini kwa likizo? Uko busy kuabudu gari lako na pesa. Hadi akizaa hakuna mahali utampeleka afurahi. Wewe ni fedheha na kicheko ndugu yangu,” shabiki huyo alimkemea Thee Pluto.
Shabiki huyo alizidi kutoa hadhari iliyojawa shubiri kwa mkuza maudhui huyo aliyejenga umaarufu kwa vipindi vyake vya mtaani almaaruf ‘Loyalty Test’
“Unamuongelesha mpenzi wako kama mzazi kwa mtoto wake mdogo. Acha nikwambie ukweli, watu watulivu ni watu wabaya sana wakati macho yao yatakapofunguka. Usimchukulie Fel poa. Unafikiri wanawake wanakupenda lakini kwa ukweli ni kwamba wanakupenda kwa pesa zako na si wewe kama wewe. Wewe ni mtu mwenye mawazo ya kinazi, tafuta uponyaji,” shabiki huyo alitema kero.
Thee Pluto alikasirishwa na maneno haya na kwenye instastories zake saa chache baadae aliamua kujibu baada ya kushindwa kuvumilia maneno haya makali yaliyomfikia kama kisu kugusa mfupa.
“Watu wengine huwa wanamjua gf wangu zaidi ya ninavyomjua. Sasa Fel mwenyewe hana shida. Sijaskia akiteta na mtu ni makasiriko anapost mtandaoni. Unaniforce nimpeleke likizo juu uliona hivi na hivyo amepelekwa. Wewe umepeleka wa kwako? Unajua mfuko wangu uko aje? Kitu ingine kwani ni kila kitu italetwa social media? Fagia kwako kwanza. Wanandoa hawa wa mtandaoni wanaungua juu ya kuchukua ushauri kutoka nje,” Thee pluto alijibu.
Kwa muda sasa mkuza maudhui huyo amekuwa akijipata katika hali ya kukunjiana mashati na mashabiki wa mitandaoni kwa kile wanasema anaonesha sana magari ya kifahari ambayo wengi wanahisi si ya kwake bali anakodisha na kujishaua nayo mitaani, huku baadhi wakimshauri ajenge nyumba kwanza na kuachana na hulka ya kuteleza na magari mazito.