Ujumbe wa Ekodydda kwa wafuasi wake baada ya kuripotiwa kupigwa na kutekwa nyara

Hapo awali, mke wa Ekodydda Cynthia Ayugi alikuwa ametangaza kwa umma kwamba ametoweka.

Muhtasari
  • Aliweka wazi kuwa hatawaruhusu wahuni wachache ambao hawaheshimu matakwa ya watu huko Mathare Kaskazini kumnyima ushindi, akiongeza kuwa kura lazima zihesabiwe wakati huu
Ekodydda
Ekodydda
Image: Instagram, KWA HISANI

Rapa maarufu wa nyimbo za injili Ekodydda amesema hataogopa vitisho baada ya kudaiwa kuvamiwa na kutekwa nyara na wapenzi wa mpinzani wake baada ya kutangazwa mshindi wa Wadi ya Mathare Kaskazini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram saa chache baada ya kuripotiwa kutoweka, rappa huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa alisema atafanya kila awezalo ili kurudisha cheti chake.

Aliweka wazi kuwa hatawaruhusu wahuni wachache ambao hawaheshimu matakwa ya watu huko Mathare Kaskazini kumnyima ushindi, akiongeza kuwa kura lazima zihesabiwe wakati huu.

Eko alibainisha kuwa mpinzani wake mkuu amekuwa akitumia majambazi kurejesha uongozi wake mbovu, jambo ambalo ameahidi kulipigania hadi mwisho.

''Nitajitahidi niwezavyo kurudisha cheti changu, ni rahisi, hatuwezi kuwaachia wahuni wachache kuendelea kulazimisha kata nzima kusaga uongozi mbaya. Kwa nini watu wanapiga kura ikiwa kura zao hazitahesabiwa? Ninawaahidi Wadi ya Mathare Kaskazini kwamba kura zenu lazima zihesabiwe mara hii,’’ aliandika.

Hapo awali, mke wa Ekodydda Cynthia Ayugi alikuwa ametangaza kwa umma kwamba ametoweka.