logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) "Nilioa Mamangu wa Kambo na Tunapendana Sana" Mwanaume asimulia

Mwanaume huyo kwa jina Umweze mwenye umri wa miaka 65 alisumulia jijsi alivyoingia katika mapenzi na mamake wa kambo pindi babake alipofariki dunia na baadae kumtolea mahari kama mkewe.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 August 2022 - 05:05

Muhtasari


  • • Baada ya kifo cha babake, waliishi na mamake wa kambo ambapo hisia za kimapenzi ziliota baina yao.
  • • Aliwafuata wazazi wa mamake wa kambo na kuwataarifu kwamba alikuwa na wazo la kumuoa mamake wa kambo na mpaka kumtolea mahari.
Mwanaume aliyemuoa mamake wa kambo

Kila sekunde iendayo kwa Mungu, dunia huwapa watu wake mambo mapya, mengine ya kustaajabisha, kuogofya, kutisha na mengine ya kukosha na kufurahisha.

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 65 amearifiwa kumuoa mamake wa kambo pindi babake mzazi alipofariki.

Kulingana na video moja iliyopakiwa kweney jukwaa la YouTube na mkuza maudhui mmoja, anaeleza kwamba mwanaume huyo kwa jina Umweze alipatwa na hisia za kimapenzi na mamake wa kambo kwa jina Nabusane, na wote walijenga hisia zao kimapenzi pindi baada ya mume wa Nabusane ambaye ni babake Umweze kufariki.

Katika video hiyo, Msimulizi anaeleza kwamba babake Umweze alioa mwanamke huyo baada ya mkewe wa kwanza kufariki na wakaishi kwa ndoa kwa miaka miwili kabla ya mzee mwenyewe kutangulia mbele za haki pia kumfuata mkewe wa kwanza ambaye ni mamake Umweze.

Baada ya kifo cha mzee, mwanaume huyo alibaki nyumbani na mamake wa kambo ambapo waliishi kwa muda peke yao, jambo ambalo linakisiwa ndilo chanzo cha hisia za mapenzi kuota baina yao.

Baada ya kugundulika kwamab wameingia katika mapenzi na mamake wa kambo, jamii iliwasuta vikali lakini mwanaume huyo alisema kwamba hajutii hata chembe kwani mapenzi yake na mamake wa kambo ni ya kudumu.

Msimulizi anasema kwamba mwanaume huyo aliwafuata wazazi wa mamake wa kambo na kuwaeleza nia yake ya kumuoa na kumfanya mkewe jambo ambalo lilipokelewa kwa mshtuko mkubwa ila mwisho wa siku wakamkubalia kutoa mahari, sharti ambalo alitekeleza na kukubaliwa kuishi na mamake wa kambo kama mkewe.

Hii hapa ni simulizi yenyewe!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved