Baada ya muungano wa Azimio la U moja One Kenya kufanikiwa katika kuwasilisha ombi lao la kutanga kubatilishwa kwa ushindi wa Ruto katika mahakama ya upeo, sasa ni wazi kwamba ni msimu wa wanasheria na mawakili tena kuoneshaba ubabe wao katika mahakama hiyo ya juu zaidi nchini.
Lakini kabla ya kumenyana rasmi katika mahakama hiyo kwa lugha na misemo changamano, inaonekana ni kama mawakili hao sasa wameanza kupasha misuli moto kwa kujibizana vikali katika mtandao wa Twitter, huku ikionekana wazi kwamba wale ambao wameteuliwa kuwakilisha mrengo wa Raila tayari wameanza kutupa mabomu moto ya maneno kwa wenzao ambao wameorodheshwa kusimama upande wa Ruto.
Juzi katika ukurasa wake wa Twitter, wakili aliyefurushwa nchini Miguna Miguna alimtania wakili mwenza gavana mteule wa Siaya James Orengo kwa kusema kwamba yeye ni wa haiba ya juu kwani anafanya masuala yake ya kisheria mpaka mahakama ya upeo nchini Canada na kusema Orengo akienda huko hata mahakama ya kesi za kawaida hawezi ruhusiwa kuwakilisha mteja.
“Kwa wale wanaouliza kama ninaweza kushinda kesi dhidi ya James Orengo, jibu langu hili hapa. Ninatekeleza sheria hadi hatua ya Mahakama Kuu ya Kanada pamoja na kuwa Wakili nchini Kenya, ilhali Orengo hawezi hata kufika katika Mahakama ya Madai Ndogo nchini Kanada,” Miguna alimshambulia Orengo kwa kejeli.
For those asking whether I can win a case against @orengo_james, here is my answer. I practice law up to the Supreme Court of Canada stage in addition to being an Advocate in Kenya, whereas @orengo_james cannot even appear at the Small Claims Court in Canada.
— Dr. Miguna Miguna (@MigunaMiguna) August 22, 2022
Huku Wakenya wakisubiri Orengo kujibu mipigo hii kwani Twitter nchini Kenya inajulikana kama jukwaa la vita vya maneno, kikundi kingine cha mawakili kimejitosa nyugani jana na kutupiana cheche za kukandiana vikali.
Baada ya upande wa Kenya Kwanza kumtaja mwanasheria Ahmed Nasir kuwa miongoni mwa wale watakaosimama upande wa Ruto kutetea ushindi wake, Wakili Ndegwa Njiru alijitoma mviringoni kwa kumshambulia mwanasheria Ahmed Nasir kuwa ana utata na mteja wake Ruto na kutaka kujua kama huku ni kuchanganyikiwa au ni sehemu ya kutoa huduma zake.
“Je, ni kweli kwamba Ahmed Nasir ana UTATA au mteja wake William Ruto amechanganyikiwa tu na huduma zake?” Njiru aliandika kwenye Twitter.
Nasir hakusita kutema moto huku akimsuta Njiru mwanzo kwa kumtaka kurejelea kamusi kujua maana halisi ya neno kuchanganyikiwa na pia kumchimba mkwara vikali kwamba alisoma masomo ya chini mengi kabla ya kuunganika kufikia masomo ya shahada ya uanasheria tena katika chuo alichokisema kilikuwa duni.
“Angalia kamusi kwa maana ya neno "kuchanganyikiwa"....hii ni kuonyesha shida zote zinazotokana na kupata "D" katika viwango vya "O"... kufanya mamia ya kozi za daraja ya kukuunganisha na digrii na kisha kufanya shahada ya sheria katika chuo kikuu ambacho kina Ofisi 3 kwenye ghorofa ya 5 ya duka la jumla mjini Kampala,” Nasir alijibu.
Is it true that @ahmednasirlaw is CONFLICTED or his client @WilliamsRuto is simply disoriented with his services?
— Ndegwa Njiru Adv. (@NjiruAdv) August 23, 2022