![](https://cms.eu-central-1.linodeobjects.com/image/2005/10/3a1lQiAAML48QJKRjn2NMrG4zoOTi7Qrz1lK89xhmn2gKrgJ-52eGJ1Ih3V_oeg5VA2OOq1WNa9V4SQWBq7bF28JeOZ2RJ-PF3ZqoCGeYcky3Ws.jpeg)
Huku nchini Kenya mdahalo bado ukiwa unazidi kurindima kuhusu haja ya wakenya kukumbatia miziki kutoka kwa wanamuziki wa humu nchini chini ya alama ya reli #Play75%KE, huko Nigeria tayari Baraza la Udhibiti wa Utangazaji la Nigeria (ARCON) limepiga marufuku wanachama wake kutumia wanamitindo wa kigeni na wasanii wa sauti kwenye vyombo vya utangazaji vya Nigeria.
Ufichuzi huu umo katika taarifa yenye kichwa, ‘Piga Marufuku Matumizi ya Wanamitindo wa Kigeni na Wasanii wa Voice-over kwenye vyombo vya Utangazaji vya Nigeria’, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo, Dk Olalekan Fadolapo, siku ya Jumatatu.
Kulingana na majarida ya nchini humo, Fadolapo alisema kuwa agizo jipya la ARCON ambalo zamani lilijulikana kama Baraza la Watendaji wa Utangazaji la Nigeria (APCON), linalingana na sera ya Serikali ya nchi hiyo yenye idadi ya watu wengi zaidi barani Afrika la kuendeleza vipaji vya ndani na ukuaji wa uchumi jumuishi kwa sekta za nchi, ikiwa ni pamoja na utangazaji.
"Kwa mujibu wa sera ya Serikali ya Shirikisho ya kuendeleza vipaji vya ndani, ukuaji wa uchumi jumuishi na haja ya kuchukua hatua muhimu na hatua zinazolenga kukuza sekta ya utangazaji ya Nigeria, Baraza la Udhibiti wa Utangazaji la Nigeria, kuwa kilele cha utangazaji, matangazo na mawasiliano ya masoko' wakala wa udhibiti wa Serikali ya Shirikisho, kwa mujibu wa mamlaka, majukumu na mamlaka yake ya kisheria kama inavyoonyeshwa na Sheria ya Baraza la Udhibiti wa Utangazaji la Nigeria nambari 23 ya 2022, inapiga marufuku matumizi ya wanamitindo wa kigeni na wasanii wa sauti kwenye tangazo lolote linalotumiwa kwenye nafasi ya utangazaji ya Nigeria kuanzia Oktoba mosi 2022,” Taarifa hiyo kwa sehemu ilinukuliwa.
BAN ON THE USE OF FOREIGN MODELS AND VOICE-OVER ARTISTS ON THE NIGERIAN ADVERTISING MEDIUM/MEDIA#arconcares#advertisingregulator#integratedmarketingcommunications pic.twitter.com/OH1yMLBxhj
— ARCON (@arconofficial) August 22, 2022
Matangazo yote, utangazaji na nyenzo za mawasiliano ya uuzaji yatafanyika kwa kutumia mifano ya Nigeria pekee na wasanii wa sauti wa nchini humo pekee. Kampeni zinazoendelea zinaruhusiwa kutimiza masharti yao. Hata hivyo, maombi yajayo ya kuthibitishwa tena kwa udhihirisho endelevu wa nyenzo kama hizo hayatatolewa na Paneli ya Viwango vya Utangazaji.
"Watangazaji, mashirika ya matangazo, vyombo vya habari, jumuiya ya watangazaji na umma kwa ujumla wanaagizwa kuzingatia." ARCON ilinukuliwa.
Nigeria imefikia hatua hiyo baada ya kugundulika kwamba vipaji vingi vya ndani ya nchi vinateketea na kutokemea kusikojulikana huku nafasi yao ikichukuliwa na vipaji vya kutoka nje ya nchi.
Nchini Kenya, msanii Eric Omondi bado angali anazidi kusukuma mswada wake bungeni unaonuiwa kuweka sheria ya kudhibiti miziki ya wasanii kutoka nje ya Kenya ambayo imefurika katika masoko yetu. Omondi anataka miziki ya wasanii wa Kenya kupewa kipaumbele cha kufaidi asilimia 75 ya kuchezwa hewani ili kuinua na kulea vipaji vingi zaidi.